Zitto alaani kifungo cha Mawio


Celina Mathew

Zitto Kabwe
MBUNGE wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema uamuzi wa Serikali kulifunga gazeti la Mawio kwa miaka miwili unapaswa kulaaniwa na kila mwanademokrasia na kwamba ni hofu.

Hivi karibuni, Rais John Magufuli alionya vyombo vya habari vinavyotaka marais wastaafu, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete kuhusishwa na sakata la mchanga wa madini.

Wakati Rais akitoa katazo hilo, juzi gazeti hilo kwenye ukurasa wake wa mbele lilichapisha picha za marais hao wastaafu   likiwahusisha na sakata la mchanga wa madini.

Pia katika ukurasa wa 12 wa gazeti hilo, yalichapishwa makala ya Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu ikionesha kuwatuhumu viongozi hao kuhusu sakata hilo huku wakiwa hawakutajwa kwenye taarifa za uchunguzi wa kamati za Rais.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Zitto alidai kuwa uhusika wa marais hao wastaafu kwenye mikataba ya madini ulisemwa na Rais Magufuli na si Mawio.

“Hakuna mkataba ulioingiwa bila Baraza la Mawaziri kuidhinisha. Kitendo cha Kamati ya Rais kutuhumu mawaziri wa zamani mbele ya Rais Magufuli na yeye kusema hatapona mtu, ilikuwa ni dhahiri kuwa Rais anawachimba watangulizi wake,” alisema. 

Alisema kwa kuwa wao ni watu waliofundishwa lugha ya uongozi, waliamua mapema kuwa Rais Magufuli alikuwa anatuhumu wenzake na kwamba gazeti hilo lilitafsiri maelezo yake.

“Kwa sisi tuliofundishwa lugha ya uongozi tuling'amua mapema kuwa Rais Magufuli alikuwa anatuhumu wenzake. Hivyo Mawio ilitafsiri tu maelezo ya Rais,”alisema na kuongeza:

“Kitendo cha Rais kuonya kuwa marais wastaafu waachwe ilikuwa ni kujisemesha tu na kufungia Mawio ni hofu ya Rais baada ya kuwasema watangulizi wake. Kila wakati Rais analia kuhujumiwa na kutaka kuombewa, adui wa Magufuli ni Magufuli mwenyewe.”

Aliitaka Serikali kulifungulia gazeti hilo mara moja bila masharti, kwani kulifunga ni kuwanyima Watanzania mawazo mbadala kuhusu mambo ya hovyo yanayoendelea nchini. 

Serikali kupitia Idara ay Habari, MAELEZO juzi ilitangaza kjulifunga Mawio kuchaowa kwa muizei 24 kuanzia juzi, kutokana na Mamlaka aliyonayo Waziri mwenye dhamana ya habari kwa mujibu wa kifungu cha 59 cha Sheria ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2016.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo