Kigwangalla akabidhi vifaa kituo cha afya


Mary mtuka

Hamis Kigwangalla
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla amekabidhi jumla ya vifaa 831 vyenye thamani ya jumla ya Sh. milioni 400, kwa kituo cha Afya Mkoani Kibaha Mjini, vifaa vilivyotolewa na Mbunge wa jimbo hilo, Silvestry Koka.

Kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, Dk. Kigwangalla alikagua maeneo ya majengo ya kituo hicho na kubaini mambo mbalimbali aliyoagiza yafanyiwe kazi ili kituo hicho kiweze kuwa Hospitali ya Wilaya.

Dk. Kigwangalla alipongeza juhudi za mbunge huyo kujali wananchi wake kwani hadi kuweza kupata vifaa hivyo aliweza kutumia maarifa na ukaribu wake na wananchi wake hivyo kufika kwa vifaa hivyo vitakuwa faraja kubwa kwa Wanakibaha na wananchi wote wa maeneo jirani.

“Nampongeza Mbunge Koka kwa kuwaletea vifaa hivi ni vizuri na vitakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Kibaha na maeneo yake ya jirani. Nakupongeza sana,” alieleza Dk. Kigwangalla.

Kwa upande wake, Mbunge huyo amemshukuru Naibu Waziri Dk. Kigwangalla kwa kuweza kufika na kujionea kituo hicho sambamba na kukabidhi vifaa huku akimuomba kuendelea kufika mara kwa mara kujionea mipango ya afya jimboni humo.

“Leo hii najisikia faraja baada ya vifaa hivi kufika  hapa jimboni kwangu kutoka nchini Marekani. Nawaomba vitumike kwa uangalifu mkubwa sana na viweze kuwa msaada kwetu,” alisema.

Alisema Halmashauri ya Kibaha imechangia Sh. milioni 32  ambazo zimesaidia usafirishaji wa vifaa hivyo kutoka nchini Marekani, huku Mbunge akitumia Sh. milioni 12 kwa ajili ya kuwaleta wataalamu kwa ajili ya ukaguzi na kuvifunga vifaa hivyo.

Mbunge huyo alisema vifaa hivyo vitagawia katika zahanati na vituo vyote vilivyopo mjini Kibaha na maeneo mengine yenye uhitaji.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo