Tumieni teknolojia ya Mawasiliano—Mtaalamu


Mary Mtuka

Teknolojia
VIJANA wametakiwa kutumia teknolojia ya mawasiliano katika kupata fursa mbalimbali, ikiwemo sera zinazoendesha nchi na hatimaye kujikwamua kimaisha.

Mwito huo umetolewa na Mgunduzi wa Mtandao wa Platform for Policy Engagement (PUPE), Farhan Yusuf katika semina ya kuwajengea uwezo vijana na kusikiliza matatizo yao mwisho mwa wiki Dar es Salam.

Alisema mitandao hiyo ikitumika ipasavyo kwa vijana ni wazi kuwa watakuwa na uwelewa mzuri na hatimae kujikwamua kiuchumi.

Yusuf alisema kutokana na changamoto kubwa ya uwelewa mdogo wa matumizi ya mitandao ameamua kuazisha PUPE ili kusainia vijana.

"Lengo langu kubwa la kuazisha mtandao huo ni kuwasaidia vijana kupata fursa ya kujifunza sera na Sheria na mambo mbalimbali yatakayo tumika katika kuiendesha nchi," alisema.

Aliongeza kuwa asilimia kubwa ya vijana wanaokaa vijiweni wamekuwa wakilalamika huku wakiwa hawajui sera wala miongozo ambayo inahusu mitandao.

Mkurugenzi Mwenza  wa  Taasisi ya Sahara  Sparks, inayojihusisha  na kuwajengea uwezo vijana katika miradi mbalimbali ya kiteknolojia, Muda Kamata  alisema wamejipanga kuwawezesha vijana hao  kuazisha mitandao mingi  zaidi.

Alisema pamoja na changamoto zinazowakabili vijana wemeona upo umuhimu wa kutumia njia ya mitandao ili kuweza kujua michanganuo mbalimbali ya kijamii kutokana na kuendelea kukuza kwa teknolojia.

Kwa upande wake Msimamizi wa Mawasiliano kutoka   Kampuni ya Teknolojia ya CIPESA, ya nchini Uganda Bassil Malaki alitumia fursa hiyo kuwa sisitiza viongozi kutumia mitandao, kwani itasaidia kutatua kero za wananchi kwa wakati.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo