Watatu Dar kizimbani kwa wizi wa kutumia nguvu


Jemah Makamba

WAKAZI watatu wa Dar es Salaam, Ramadhan Salum (18), Bakari Ally (18) na Ibrahim Ally (19) wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa tuhuma za wizi wa kutumia nguvu.

Akiwasomea mashitaka watuhumiwa hao jana mbele ya Hakimu John Msafiri, mwendesha mashitaka Sylvia Mitanto alidai walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha sheria cha 286 sura ya 16 kama kilivyorekebishwa mwaka 2002.

Ilidaiwa kuwa Aprili 21 maeneo ya Gongolamboto watuhumiwa hao walimvamia Irene Shayo na kabla na baada ya kumwibia mkoba walimpiga na kumsababishia maumivu mwilini.

Washtakiwa hao walikana mashitaka na mwendesha mashtaka kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Hakimu Msafiri aliwapa washitakiwa hao masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika, mmoja akiwa na ajira kwenye taasisi inayotambulika na wasaini dhamana ya Sh 400,000.

Washitakiwa walishindwa kukidhi masharti ya dhamana na Hakimu Msafiri kuamuru warudishwe rumande hadi Julai 12 kesi hiyo itakapotajwa.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo