Dalila Sharif
Mimba za wanafunzi |
TAASISI
ya James Foundation imetangaza kuunga mkono msimamo wa Serikali wa
kutowarejesha shuleni wanafunzi wanaopata ujauzito wakiwa.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo ya kiraia inayojuhusisha
na masuala ya kijamii, Leornad Manyama alisema ni vema kumwunga mkono Rais John
Magufuli katika suala hilo ili kudumisha malezi ya maadili mema na heshima kwa
mwanafunzi.
Julai 23,
Rais Magufuli akiwa Bagamoyo kwenye ziara ya kikazi mkoani Pwani, alitoa
msimamo huo wa Serikali wa kutorudisha shuleni wanafunzi watakaopata mimba
wakiwa shule za msingi na sekondari hasa zinazomilikiwa na Serikali.
“Sisi
taasisi tumetafakari kauli ya Rais na kujiridhisha bila shaka hatua yake na Serikali
kuwa ina malengo ya kulinda maadili ya Taifa na uwajibikaji kwa watoto, vijana,
wazazi, walezi na jamii kwa jumla,” alisema Manyama.
Alifafanua
kuwa kama Taifa, kuacha wanafunzi wajihusishe na mapenzi na kupata ujauzito na
wakishajifungua warudi shuleni, itasababisha kupunguza misimamo, maadili na
kujikita katika tabia mbovu zisizo za kimaadili.
“Ili
kulinda maadili, ni lazima kila Mtanzania kusimamia agizo la Rais na
kulitekeleza ili kuwapa elimu watoto watambue kuwa wakifanya hivi hakuna
kuendelea na masomo, na hali hii itasaidia kupungunza mimba kwa wanafunzi shuleni,”
alisema Manyama.
Aidha, alisema
taasisi yake inaunga mkono agizo la Rais katika kulinda maadili ya Taifa kwa
kuandaa kongamano la kutembelea wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari mikoani
kwa kushirikiana na wazazi ili kutoa mada za maadili na malezi, ili kutokomeza
mimba kwa wanafunzi.
Pia
taasisi hiyo ilionya viongozi au watu wanaopinga kauli ya Rais kwa lengo la kupoteza
wanafunzi na kuwachochea katika kukuza upataji mimba shuleni.
0 comments:
Post a Comment