Msimamo wa JPM waungwa mkono


Dalila Sharif

Mimba za wanafunzi
TAASISI ya James Foundation imetangaza kuunga mkono msimamo wa Serikali wa kutowarejesha shuleni wanafunzi wanaopata ujauzito wakiwa.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo ya kiraia inayojuhusisha na masuala ya kijamii, Leornad Manyama alisema ni vema kumwunga mkono Rais John Magufuli katika suala hilo ili kudumisha malezi ya maadili mema na heshima kwa mwanafunzi.

Julai 23, Rais Magufuli akiwa Bagamoyo kwenye ziara ya kikazi mkoani Pwani, alitoa msimamo huo wa Serikali wa kutorudisha shuleni wanafunzi watakaopata mimba wakiwa shule za msingi na sekondari hasa zinazomilikiwa na Serikali.

“Sisi taasisi tumetafakari kauli ya Rais na kujiridhisha bila shaka hatua yake na Serikali kuwa ina malengo ya kulinda maadili ya Taifa na uwajibikaji kwa watoto, vijana, wazazi, walezi na jamii kwa jumla,” alisema Manyama.

Alifafanua kuwa kama Taifa, kuacha wanafunzi wajihusishe na mapenzi na kupata ujauzito na wakishajifungua warudi shuleni, itasababisha kupunguza misimamo, maadili na kujikita katika tabia mbovu zisizo za kimaadili.

“Ili kulinda maadili, ni lazima kila Mtanzania kusimamia agizo la Rais na kulitekeleza ili kuwapa elimu watoto watambue kuwa wakifanya hivi hakuna kuendelea na masomo, na hali hii itasaidia kupungunza mimba kwa wanafunzi shuleni,” alisema Manyama.

Aidha, alisema taasisi yake inaunga mkono agizo la Rais katika kulinda maadili ya Taifa kwa kuandaa kongamano la kutembelea wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari mikoani kwa kushirikiana na wazazi ili kutoa mada za maadili na malezi, ili kutokomeza mimba kwa wanafunzi.

Pia taasisi hiyo ilionya viongozi au watu wanaopinga kauli ya Rais kwa lengo la kupoteza wanafunzi na kuwachochea katika kukuza upataji mimba shuleni.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo