Kigwangalla akemea kazi za mazoea


Mwandishi Wetu

Dk. Hamisi Kigwangalla
NAIBU Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla amehimiza watumishi wa Wizara yake kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuzingatia sheria, miongozo, taratibu na maelekezo ya kazi.

Akiwa kwenye ziara ya Mtwara, juzi alielekeza watumishi hao kuwa dhamana waliyopewa kuhudumia wananchi wenzao ni kubwa, hivyo hawana budi kuzingatia kanuni za afya ili kuepuka maambukizi yatakayotokana na uzembe.

Aliwataka kulipa kipaumbele suala la usafi wa mazingira, vifaa na maeneo yote wanayofanyia kazi hususan uhifadhi wa taka za hospitali katika utaratibu maalumu unaozingatia mfumo wa kinga na udhibiti wa taka. 

Miongoni mwa mambo aliyobaini katika ziara hiyo ni ubovu wa baadhi ya vifaa tiba katika maabara na vyumba vya upasuaji na kuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, kuchunguza mikataba yote ya usambazaji vifaa tiba na matengenezo.

Aidha, Dk Kigwangalla alibaini baadhi ya vifaa vya kisasa vilivyo kwenye vituo hivyo havitumiki ipasavyo, kwa sababu watumishi waliopo hawana ujuzi wa kuvitumia na alimwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa kulishughulikia tatizo hilo haraka kwa kuwajengea uwezo wataalamu hao.

Mbali na kujionea hali hiyo, Dk Kigwangalla pia alitoa maagizo kwa watendaji wa vituo na viongozi wa wilaya husika kuhakikisha wanasimamia ipasavyo utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.

Dk Kigwangalla akiwa Mtwara, alitembelea zahanati, vituo vya afya na hospitali, kati hizo kuwa ni:  Kituo cha Afya Mahurunga, cha Nanguruwe na zahanati ya kijiji cha Dinyecha.

Pia alitembelea Hospitali ya Wilaya ya Newala na Kituo cha Afya cha Newala DC, zahanati ya Lulindi, ya Nagaga, hospitali ya Halmashauri ya Masasi-Mkomaindo na zahanati ya Mbonde.

Aidha, aliendelea na ziara yake Ruvuma ambako  atatatembelea vituo vya afya na hospitali za mkoa huo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo