Mbunge CUF akunwa na Magufuli


Mwandishi Wetu

Rais John Magufuli
MBUNGE wa Mtwara Mjini, Maftaha Nachuma (CUF), ametaja baadhi ya mambo katika 34 yaliyomfanya kupiga kura ya ‘ndiyo’ kwenye mchakato wa upitishaji Bajeti kwa mwaka 2017/18.

Baadhi mambo hayo ni pamoja na Bajeti kutetea rasilimali za madini, kuondoa kodi kwenye maeneo mengi yanayogusa wananchi na kuondoa tozo zilizokuwa zikitesa wafanyabiashara.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Nachuma alisema kwa kiasi kikubwa kuoendolewa tozo kwenye mazao kutawezesha upatikanaji chakula kwa wingi na bei haitapanda.

“Mimi mbunge ninayejitambua, nampongeza Rais John Magufuli kwa kusimamia rasilimali za nchi vizuri licha ya kuwapo watu wasio na sera wanaoponda anavyofanya, hivyo namsihi akaze buti,” alisema.

Aliongeza kuwa anaunga mkono bajeti zote zilizopitishwa pamoja na mikataba ya madini iliyosainiwa na kupitishwa na Serikali ya sasa.

Aidha, alisema mambo mengine katika hayo 34 anatarajia kuyataja katika mikutano yake ya hadhara anayotarajia kuifanya jimboni hivi karibuni.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo