Lowassa: Nitamtafuta Magufuli



WAKATI Chadema jana ikiamua kuahirisha kuanza mikutano na maandamano yasiyo na ukomo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Edward Lowassa amesema atamtafuta Rais John Magufuli wa­zungumze.

Hatua hiyo ilifikiwa jana na chama hicho cha Upinzani kwa ilichokieleza ni kuheshimu mwito wa viongozi wa dini walioomba ku­pewa nafasi ya wiki mbili ili wazun­gumze na uongozi wanachi.

Wakati uamuzi huio uklifikiwa nakutangazwa, Lowassa alielezea kukutana kwake na Rais Magufuli siku ya maadhimishio ay Jubilei ya miaka 50 ya ndoa ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Alioserma siku hiyo wawiklin hao hawakuzungumza mambo maui­ubwa zaidi ya kusdalimiana na ku­peana mikonmo na kujuliana hali, hivyio kuwapo haja ya kukuitanma nma kluzungumza kwa kina. Lowassa alisema jana kuwa baada ya kusalimiana walipotana Rais Magufuli alimwambia kwamba atamtafuta.

“Nimeona mitandao imeandika mambo mbalimbali lakini kusema ukweli hakuna jambo lolote ambalo tumezungumza na Magufuli tofauti na salamu na kuniambia kuwa atanitafuta,” alisema.

Kuhusu kusalimiana naye alisema hakuwa na nguvu yoyote ya kumkatalia au kutomsalimia hasa ukizingatia katika tukio hilo kulikuwa na viongozi wa kiroho.

“Nadhani nyie ni wenzangu na mnaamini katika imani hivyo sikuwa na nguvu ya kukataa mkono wa Rais mbele ya viongozi wa dini sijui nyie,” alisema.

UKUTA
Wakati huo huo, Chadema kimeahirisha maandamano na mikutano iliyopanga kuanzia leo nchi nzima kikieleza kutii viongozi wa dini waliooomba wapewe wiki mbili ili kuonana na Rais John Magufuli, kutatua mgogoro uliopo.

Kabla ya kuahirishwa maandamano hayo, Julai 26 Chadema kupitia Kamati Kuu ilijitokeza mbele ya waandishi wa habari na kutangaza operesheni hiyo ilijulikana kwa jina la Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta), ambao umeweza kuwa gumzo katika nchi nan je ya nchi.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe alisema viongozi wa dini wa madhehebu yote makubwa hapa nchini, taasisi za kiraia, balozi na vyombo vya habari wamewaomba wasitishe.

Mbowe alisema viongozi hao ni  Mkuu Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Mkuu wa Kanisa la Afrika Inland Tanzania, Katibu Mkuu wa Baraza Kikrustu Tanzania, Mkuu wa Kanisa la Kipentakosti Kirismatiki Tanzania, Mufti Mkuu wa Tanzania na Mufti Mkuu wa Zanzibar.

Aidha, alisema viongozi wa taasisi za kiraia kama Kituo cha Haki za Binadamu Tanzania (LHRC), Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Jukwaa la Katiba na Jukwaa la Wahariri na wengine wengi wamewaomba watoa muda wa wiki mbili ili kutoa sintofahamu.

Alisema katika mazingira hayo ya taasisi na viongozi wa dini wamelazimika kuahirisha hadi Oktoba mosi iwapo hakutakuwa na muafaka.

Mbowe alisema mgogoro huo wa kisiasa unatokana na uvunjifu wa Katiba unaofanywa na Rais John Magufuli na vyombo vyake vya dola hivyo hawapo tayari kukubaliana nao.

Alisema haki zao za kisiasa zimetajwa katika Katiba hivyo ni wazi kuwa hawapo tayari kuona haki hiyo ikipotea na kwamba wapo tayari kuondoa tofauti zao kwa njia ya mazungumzo.

“Sisi Chadema hatuwezi kuwakaidi viongozi wetu wa dini kwa sababu yoyote kwani ni aibu kwa sisi kufanya hivyo hasa ukizingatia tumelelewa na imani hivyo basi tunaahirisha maandamano hadi Oktoba mosi iwapo hakutakuwa na muafaka,” alisema.

Mbowe alisema wanaomba wadau na makundi mbalimbali kushirikiana na Chadema katika kupinga vitendo hivyo kwani kitendo hicho kinaumiza kila mtu.

Alisema iwapo Rais Magufuli ataachiwa nafasi ya kukanyaga Katiba hakuna ambaye atapona au kuwa salama.

Mwenyekiti huyo alisema katika kipindi kifupi cha Rais Magufuli kiburi na dharau imeonekana kutoka kwake na watawala wengine badala ya kukaa na kuzungumza mema ya nchi hii ikiwemo amani.

Alisema viongozi hao wanahubiri amani lakini matendo yao yanashiria uvunjifu wa amani na kinyume chake ni kuandaa majeshi na kutesa viongozi, wanachana na watu wote ambao wapo kinyume na mitizanmo yao.

Mbowe alisema uamuzi huo unaweza kuwasikitisha wanachama wao lakini hakuna sababu ya kuingiza nchi katika mgogoro ambao hauna sababu hivyo kuwataka wasubiri mazungumzo ya viongozi.

‘Hatuachi kuandamana kesho kwa sababu ya Jeshi la Polisi au Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ila tumekubaliana kuheshimu viongozi wetu wa dini pamoja na ukweli kuwa rais anawadharua, lakini ikifika Oktoba mosi tutaendeleza harakati zetu za kudai haki,” alisema.

Kwa upande mwingine Mbowe alisema katika kipindi cha mwezi mmoja wa maandalizi ya Ukuta viongozi na wanachama 230 wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka maeneo mbalimbali nchini.

Halikadhalika alisema wabunge wa Chadema, watarudi bungeni baada ya ombi la viongozi wa dini na kuwa wanatarajia kukutana Dodoma kutafakari ushauri huo ili wawe na kauli moja ya kurejea.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo