Viongozi wataka suluhu ya Ukuta



KIONGOZI wa dini na viongozi wa makabila wamejitokeza kutaka suluhu katika mgogoro unaoendelea baina ya Chadema kwa upande mmoja na Serikali na Polisi kwa upande mwingine.

Askofu wa Jimbo Katoliki la Dodoma, Mhashamu Beatus Kinyaiya ametaka viongozi wa Chadema kutumia uhuru walionao vizuri kukaa na Serikali meza moja kuelewana badala ya kuhamasisha vijana washiriki maandamano ya Operesheni UKUTA yanayotarawa kufanyika Septemba mosi.

Alisema jana kwamba kama yatafanyika, upo uwezekano mkubwa maandamano hayo yakasababisha madhara makubwa kwa jamii ya Watanzania. Askofu huyo alitoa kauli hiyo alipozungumza na JAMBO LEO, baada ya kumaliza kutoa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara kwa watoto 111 wanafunzi wa shule ya Martin Luther mjini Dodoma.

“Kwa kuwa washiriki wenyewe wa maandamano wengi ni vijana, kunaweza kutokea madhara mengi yakifanyika. Tunajua kila Mtanzania ana uhuru wa kufanya kitu anachokifikiri kutokana na uhuru uliopo nchini,” alisema na kuongeza:

“Lakini naomba viongozi wa Ukawa kuutazama na kuutumia vizuri uhuru huo, hasa kukaa meza moja na Serikali wakaondoa tofauti zilizopo.”

Alisema moja ya madhara yanayoweza kujitokeza ni vijana wasio na nia nzuri kujiingiza kwenye maandamano hayo, kisha kusababisha fujo, hali inayoweza kuathiri utendaji kazi katika maeneo mengi na hasara kujitokeza kwa kuwa yanasemwa ni ya nchi nzima.

“Kwanza nasema kwa sababu ni Watanzania, kila mtu ana uhuru wa kufanya atakacho lakini ni vema kama wangekutana na Serikali wakazungumza wakalimaliza mapema kuliko kuacha mpaka wafike huko ambapo kunaweza kusababisha hasara kubwa,” alisema Kinyaiya na kufafanua:

“Vijana ni vijana, kwenye hayo maandamano yao wanaweza kuanza vizuri,†lakini vijana wenzao walio na nia mbaya wanaweza kijichomeka na wakasababisha fujo.”

Kuhusu hali ya kisiasa nchini, Askofu Kinyaiya alisema kutokuwa na mazungumzo ya kutosha kati ya vyama vya siasa na Serikali kunasababisha vuguvugu la kutazamana vibaya, hivyo ili kuondoa ukakasi huo kuwe na maelewano kati yao.

Shekhe Alhad

Katika hatua nyingine, Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ametoa mwito kwa viongozi wa kisiasa nchini, kuwa wavumilivu ili kulinda amani ya nchi.

Shekhe Alhad alisema hayo jana ofisini kwake, Dar es Salaam akitaka viongozi hao kutii Mamlaka iliyopo kwani imewekwa na Mungu na hivyo ni vema kutafuta njia nyingine kumaliza matatizo yanapotokea.

“Ipo haja ya kuvumiliana kwa ajili ya Taifa letu, kwani yanapotokea machafuko waathirika wakubwa ni wanawake, watoto na vijana wetu ambao wanaweza kupata madhara makubwa na hata kupoteza maisha,ííalisema Alhad.

Akizungumzia maandamano ya Ukuta yaliyopangwa kufanyika Septemba mosi, alisema kauli ya kuzuia maandamano hayo ilitolewa na Rais wa Nchi na kuomba ipewe uzito wa kipekee, kwani busara ni kusikiliza Mamlaka imesema nini na kutii kauli hiyo ya Rais.

“Nawashauri Watanzania wenzangu, viongozi wangu wa kisiasa jambo hilo si vyema tukashiriki kwani kutotii Mamlaka ni dhambi ndivyo vitabu vya dini vinanavyosema,íí alifafanua Shekhe Alhad.

Wazee Nao 
wazee wa jamii ya kimasai wameiomba Serikali kukaa mezani na wanasiasa wanaounda Operesheni Ukuta ili kumaliza hali inayojitokeza hivi sasa.

Akizungumza kwa niaba ya jamii hiyo, Kiongozi Mkuu (Laibon), Masaine Kumunyu alisema hawako tayari kushiriki jambo hilo kwani wanaitii Serikali. Alisema kwa muda mrefu kumekuwa na malumbano kati ya viongozi wa kisiasa na Serikali ambapo walisema kuna mambo wanaona hayafanyiki vema.

“Sisi Wamasai hatuwezi kushiriki maandamano hayo, lakini pia tunaomba pande hizi kwa maana ya Serikali na viongozi wa vyama vya kisiasa kukaa mezani ili kuzungumzia mambo hayo na kuepusha madhara siku hiyo, Serikali inakataza, wanasiasa wanasema azma iko palepale, kwa hali hiyo tunaziomba pande mbili hizi kukaa mezani kuzungumza,” alisema Kumunyu.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo