Tulia: Wabunge wote ni sawa

NAIBU Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson amesema hakuna mbunge mwenye hadhi ya juu kuliko mwingine katika Bunge na kwamba Katiba inatambua na kueleza kuwa wabunge wote wapo sawa.

Aidha alisema katika utendaji wake hana upendeleo kwa mbunge yoyote bali hutekeleza wajibu wake kwa kufuata sharia na kanuni zinazoliongoza Bunge.

Akizungumza kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha ITV, Dk. Tulia alisema makundi yote ya wabunge yakishaapishwa huwa ni wabunge wanaofanana kwa hadhi ya kufanya kazi wanapokuwa bungeni.

“Katiba ilivyoyaweka makundi matano ya wabunge kuanzia wanaoteuliwa na Rais, wanaochaguliwa na wananchi, wabunge wa viti maalum na wanaotoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wote wamewekwa kwa sababu maalumu kwa sababu hiyo wabunge wote ni sawa," alisema Dk. Tulia

Aidha Naibu Spika ameitaka jamii kubadilika kutoka katika dhana kwamba mwanamke ambaye anashika nafasi ya juu katika uongozi kwamba amebebwa na waamini kuwa vigezo na masharti vinazingatiwa.

“Wanawake wengi ambao wamepewa nafasi ya uongozi kwa kuchaguliwa au kuteuliwa ni mara chache sana hufanya vibaya na hata akifanya vibaya jamii humhukumu kwa kuwa ni mwanamke wakati kuna wanaume katika nafasi kama hiyo ambao pia unakuta wamefanya vibaya hivyo kuna changamoto hiyo katika jamii," alisema.

Katika hatua nyingine alisema anaongoza Bunge bila upendeleo wowote ila anafuata sheria na kanuni za kuongoza Bunge.


Pia alizungumzia tatizo la upnde wa wabunge wa upindani kutoka nje bunge likiwa linaendelea ambapo alisema "katika hali ya kawaida ukiwa kiongozi lazima ujifunze kuishi na watu wa kila aina, wakiwa pale ndani wakiwa kundi wakitoka ndo mtu unaona sijui wamefanyaje, lakini mimi ndiye ninayeshughulika na mambo yao ya kila siku ofisini pale.”
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo