Na William Shao
Chakumb,a klsd lashds dash djkhsad askdgsa dgjksadsajk |
Baraza la
Kuhifadhi Mali za Asili la Marekani linasema kwamba asilimia 40 hivi ya chakula
chote nchini humo hakitumiwi. Kwa mfano, inakadiriwa kwamba asilimia 7 ya mazao
yote hayavunwi, kwamba asilimia 17 ya vyakula vya mikahawani haviliwi, na
kwamba familia hutupa asilimia 25 hivi ya vyakula wanavyonunua.
“Taifa letu linapaswa kujifunza mambo
mengi ambayo kwa sasa yanatendeka barani Ulaya," likasema jarida 'European Parliament News' la January
19, 2012. Uingereza na Jumuiya ya Ulaya wamefanya utafiti ili kuelewa
kinachosababisha tatizo hili.
Januari 2012, kwa mujibu wa jarida 'European Parliament News', Bunge la
Ulaya lilipitisha azimio la kupunguza taka za vyakula kwa asilimia 50 ifikapo
mwaka 2020 na kuutaja mwaka 2014 kama "Mwaka
wa Ulaya Dhidi ya Taka za Vyakula". Mwaka huo, 2014, Uingereza
ilifanya kampeni iliyojulikana kama "Penda
Chakula, Chukia Taka."
Kwa mujibu wa Idara ya Kilimo ya
Marekani (USDA), kaya pamoja na
wafanyabiashara wa chakula kama mahoteli na migahawa, kwa pamoja ziliharibu
chakula cha thamani ya zaidi ya paundi bilioni 86 za Uingereza (sawa na Tsh.
245,775,740,000,000) kwa mwaka 2008 pekee, au asilimia 19 ya chakula chote
kilichosambazwa nchini Marekani kwa mwaka huo. Hiyo ni kwa mujibu wa jarida ‘The Journal of Consumer Affairs’ chini
ya makala “The Value of Retail- and
Consumer-Level Fruit and
Vegetable Losses in the United States.
“Asilimia 40 ya
chakula chote kinachonunuliwa kwa ajili ya hoteli na migahawa kinatupwa kabla hakijamfikia
mlaji,” linasema jarida USDA Food Review
la Marekani na kuongeza kuwa kiasi kingine cha chakula “…kinahifadhiwa lakini
hakiliwi…” hadi kinakuwa taka.
0 comments:
Post a Comment