Ukataji miti unaongeza malaria



Ukataji wa miti katika misitu ya kitropiki umechangia ongezeko la malaria kwa asilimia 50 hivi. Hivyo ndivyo wanavyosema watafiti fulani ambao wamekuwa wakichunguza habari kutoka wilaya 54 za nchini Brazili, pamoja na picha za satelaiti zinazoonyesha shughuli za ukataji miti.

Malaria inasambazwa sana katika eneo hilo na mbu anayejulikana kama Anopheles darlingi. Huyo ni aina ya mbu anayeeneza malaria kwa wingi katika ukanda wa kitropiki wa Mexico na kusini mwa eneo hilo.

Sarah Olson, aliyeandika ripoti hiyo anasema, “Eneo lililokatwa miti na kuachwa wazi na lenye vidimbwi vya maji vinavyopata kiasi kidogo cha mwanga wa jua, huandaa mahali pazuri pa mbu hao kuzaana.” Maeneo ambayo yaliyoripotiwa kuwa na visa vingi vya malaria ni yale yaliyokatwa miti.

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Wisonsin-Madison nchini Marekani walijiuliza, “Kukata mti mmoja katika Msitu wa Amazon kunamaanisha chochote kwa mbu anayeeneza malaria?” Baada ya utafiti wao wakapata jawabu la “NDIYO”.

Watafiti hao waligundua kuwa kitendo cha kupungua kwa asilimia nne ya mistu ya mvua kumesababisha ongezeko la asilimia 50 la visa vya malaria magharibi mwa Brazil, na hali ilikuwa hivyo mwongo baada ya miti kuwa imekatwa.

Timu ya watafiti hao iligundua kuwa ukataji wa miti ulikuwa unajenga mazingira bora kwa aina hiyo ya mbu ambao hupendelea sana sehemu yenye mwanga wa jua.

Utafiti mwingine uliochapishwa katika tovuti ya Kituo cha Kinga na Udhibiti wa Afya cha Marekani ulisema: “…kuna uhusiano mkubwa kati ya ukataji miti na ongezeko la malaria…”

Kwa mujibu wa taarifa ya Taasisi ya Kimataifa ya Afya, mtafiti wa afya ya mazingira, Jonathan Patz, alikaririwa akisema: “Kama wizara za afya za nchi waathirika hazitafanya kazi pamoja kuzuia hili (ukataji miti), kamwe hatutapata suluhisho … tutakuwa tunatafuta suluhisho la juu juu tu.”

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo