Wainjilisti waimwagia pongezi Serikali


Hussein Ndubikile
UMOJA wa Wainjilisti wa Kikristo Tanzania (Uwakita) umeipongeza Serikali kwa kazi nzuri inazoendelea kufanya, ikiwemo kusimamia nidhamu ya kazi, kutetea wanyonge, kukusanya kodi, kupambana na ufisadi na kuhamasisha usafi wa mazingira.

Mjumbe wa umoja huo, Elieza Shinza alisema tangu Rais John Magufuli achaguliwe kuiongoza nchi, amekuwa mstari wa mbele kusimamia nidhamu ya watumishi wa umma na uwajibikaji.

“Tunapenda kumpongeza Rais Magufuli na Serikali yake kwa kazi anazozifanya. Anatetea wanyonge, anasimamia ukusanyaji kodi na kupambana na ufisadi,” alisema.

Alisema rais Magufuli ni kiongozi wa kuigwa kutokana na msimamo alionao wa kuwapigania watu wa hali ya chini na kuvikataa vitendo vya rushwa ndani ya Serikali.

Katika hatua nyingine, umoja huo umeomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu ziara ya mfalme, Mohamed VI wa Morocco iliyofanyika nchini mwishoni mwa mwaka jana ilikuwa ni ya Kiserikali au ya kidini.

Shinza alisema ombi la ufafanuzi huo limetokana na kwamba kiongozi huyo anatambulika kama kiongozi wa Kiserikali na kiongozi mkuu wa dini katika nchi yake, hivyo ni vyema suala hilo likafafanuliwa kuondoa utata uliojengeka.

Alisema licha ya kusainiwa mikataba ya kimaendeleo baina ya nchi hizo, huku akiongeza rais Magufuli aliutangazia umma kuwa amemwomba mfalme huyo kumjengea msikiti jijini Dar es Salaam na kwamba ilikuwa halali kwa rais kufanya hivyo.

Aliongeza kuwa Uwakita unaomba kufahamu kuwa rais kuomba kujengewa msikiti ni kipaumbele cha nchi.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo