Majaliwa ataka mvua zitumike vizuri


Christina Nkya, Dodoma

Kassim Majaliwa
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, ametaka wananchi kutumia vizuri mvua zinazonyesha nchini, kulima mazao ya muda mfupi, ili kukabiliana na uhaba wa chakula katika baadhi ya maeneo nchini.

Alitoa ushauri huo juzi alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Magu, Kiswaga Desideri (CCM), katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu.

Desideri alitaka kujua Serikali inachukua hatua gani kukabiliana na uhaba wa chakula.

Katika hatua nyingine, Majaliwa alisema Serikali inaendelea kuimarisha viwanda vya ndani, ili vizalishe sukari kwa wingi kuepuka upungufu wa bidhaa hiyo kama uliotokea mwaka jana.

Akijibu swali la Mbunge wa Mvomero, Suleiman Sadik (CCM), Majaliwa alisema Serikali haitarajii kuwapo upungufu wa sukari nchini kama ilivyokuwa mwaka jana, kwa sababu viwanda vya ndani vimeanza uzalishaji na vinaendelea kuzalisha.

Katika swali lake, Sadik alisema mwaka jana nchi ilikumbwa na uhaba wa sukari uliosababishwa na uzalishaji mdogo wa viwanda vya ndani na kutaka maelezo kuhusu hatua za Serikali kukabiliana na hilo.

“Napenda kujua hali ya upatikanaji wa sukari kwa sasa ikoje nchini na Serikali imejiandaaje kukabiliana na uhaba huo ili usitokee kama mwaka jana,” alisema Sadik.

Akifafanua Majaliwa alisema kwa taarifa zilizopo hadi Machi, nchi itakuwa imefikia malengo ya uzalishaji kwa sababu mwishoni mwa Januari, uzalishaji ulifikia asilimia 86 ya mahitaji.

Hata hivyo, alibainisha kuwa kukitokea upungufu wa sukari Serikali itachukua hatua ya kukabiliana nao.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo