Bunge latilia shaka matumizi kwenye miradi


Fidelis Butahe, Dodoma

KAMATI ya Bunge ya Katiba na Sheria imebaini matumizi ya fedha za umma yasiyoridhisha kwenye baadhi ya miradi nchini.

Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais mtaa wa Luthuli, Dar es Salaam, kwa maelezo kuwa limejengwa chini ya viwango.

Kwa hali hiyo, Kamati imezitaka mamlaka husika kufanya uchunguzi ili kujiridhisha na matumizi ya fedha za mradi huo na hatua zichukuliwe kwa watendaji waliohusika na mradi huo.

Akizungumza wakati akiwasilisha taarifa ya Kamati hiyo bungeni jana, Mwenyekiti wake, Mohamed Mchengerwa alisema Kamati ilifanya ziara kwenye jengo hilo na kubaini kujengwa chini ya kiwango, “watendaji wote waliohusika wachukuliwe hatua kali.

“Pia ujenzi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Serikali imekuwa ikiomba fedha Sh bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hiyo kwa miaka mitatu mfululizo.”

Alisema licha ya fedha hizo kuombwa kuanzia mwaka 2014 hadi mwaka jana, ofisi hiyo haikupokea kiwango chochote kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Kuhusu miradi ya Dege Eco, Kigamboni, Mchengerwa alisema ripoti ya uchunguzi wa miradi ya Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), ukiwamo mradi huo ipo katika hatua za mwisho kukamilishwa na taasisi zinazofanya uchunguzi.

“Kamati ilitoa muda kwa Serikali kukamilisha ripoti hizi na inatazamia kupewa taarifa kamili za uchunguzi huu,” alisema Mwenyekiti wa Kamati.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo