Kizimbani akidaiwa kuwatukana JPM, Samia


Grace Gurisha

MTUNZA Bustani, Maganga Masele (25), amefikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akituhumiwa kutoa lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kuhusu utendaji wao wa kuliongoza Taifa.

Wakili wa Serikali, Lucy Maliya alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage kuwa Desemba 22 mwaka jana, Masele akiwa Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam alitoa lugha ya matusi dhidi ya Rais Magufuli na Samia, maneno ambayo yangeweza kuleta uvunjifu wa amani.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Masele alikana kuhusika na tuhuma hizo, ambapo Maliya alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, pia hakuna pingamizi la dhamana kwa kuwa kisheria kosa hilo linadhaminika.

Hakimu Mwijage alisema ili mshitakiwa awe nje kwa dhamana, anatakiwa awe na mdhamini mmoja mwenye barua ya utambulisho atakayesaini bondi ya Sh 500,000.

Masele alikamilisha masharti hayo na kuachwa kwa dhamana, na kesi yake itatajwa Januari 24.  

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo