Mahakama yakwama kuamua kesi ya bilionea Msuya


Grace Gurisha

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imeshindwa kutoa uamuzi kama itafuta shtaka la mauaji dhidi ya mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Msuya (41) au la, anayeshtakiwa kumuua dada wa marehemu huyo, Aneth ikianisha sababu za kushindwa kufanya hivyo.

Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Godfrey Mwambapa aliahirisha kesi hiyo jana hadi Desemba 21 mwaka huu kwa sababu bado hajamaliza kuandika uamuzi huo ambao umekuwa ukiahirishwa mara kwa mara kutokana na sababu mbalimbali za kimahakama.

Hatua hiyo imefikiwa na mahakama hiyo, baada ya Wakili wa Miriam, Peter Kibatala kuwasilisha ombi hilo mbele ya Hakimu Mkazi, Magreth Bankika wa mahakama hiyo kuwa hati ya mashtaka ina kasoro na kuomba ifutwe, pia akidai kuwa wateja wake waliteswa na polisi.

Mbali na Miriam, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara wa Jiji la Arusha, Revocatus Muyela (40). Kibatala alidai pia kuwa washtakiwa hao waliteswa na askari kabla ya kuchukuliwa maelezo ili wakiri kuhusika na mauaji hayo.

Akijibu hoja hizo, Wakili wa Serikali, Diana Lukondo alisema hati ya mashtaka iliyokuwa mbele ya mahakama iko sahihi kwani ina sababu zote za kuitwa hati ya mashtaka, hivyo hoja za Kibatala hazina mashiko.

Muyela aliunganishwa katika kesi hiyo, baada ya kukamatwa na kubainika kuwa na yeye anatuhumiwa katika mauaji hayo.

Aneth alikuwa dada wa marehemu bilionea Msuya, alichinjwa na watu wasioulikana nyumbani kwake Kibada, Block 16, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Mei 26, mwaka huu.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo